1
1
Tathmini ya awali inaonesha hisa za makampuni yanayoratibu safari zimeporomoka kwa zaidi ya dola bilioni 22 kutokana na kufungwa kwa viwanja vikubwa vya ndege vya eneo la ghuba na kuongozeka kwa gharama za nishati.
Siku ya Jumatatu Machi 02, pipa moja la mafuta ghafi lilifikia dola 82 ambayo ni ongezeko la asilimia 13 ikilinganishwa na bei ya wiki iliyopita.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Anga lenye makao yake mjini Montreal, Canada, limesema mataifa duniani yana wajibu wa kuhakikisha usalama wa safari za ndege ili kupunguza hasara inayoshuhudiwa.