1
1
Diaz-Canel ameyasema haya wakati wa mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya watu kwa ajili ya kuadhimisha miaka 65 ya azimio la Mapinduzi ya Kisoshalisti ya Cuba.
Rais huyo ameyasema haya huku mivutano ikizidi kati ya nchi hizombili na mgogoro wa Cuba ukiendelea kuwa mbaya zaidi kutokana na vizuizi vya nishati vya Marekani.
Mapema wiki hii, utawala wa Trump ulisema kuwa unaweza kuigeukia Cuba mara tu vita dhidi ya iran vitakapofika mwisho.
Awali Trump alitishia kuwa ataivamia Cuba kama jeshi la Marekani lilivyofanya Januari huko Venezuela na kuzuia usafirishaji muhimu wa mafuta kutoka nchi hiyo ya kusini mwa Amerika.
CHANZO: DW SWAHILI