Popular Posts

Iran yaipa Pakistan masharti ya mazungumzo na Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi akiwa mjini Islamabad Jumamosi Aprili 25,2026 amewasilisha kwa Pakistan masharti ya nchi yake kuhusu mazungumzo ya usuluhishi na Marekani.

Chanzo kinachohusika na majadiliano hayo kutoka Pakistan kimesema Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Iran ameorodhesha pia masuala yenye utata katika matakwa ya Marekani kwenye mazungumzo hayo. Hayo ni kulingana na chanzo kutoka Pakistan ambayo ndiyo msimamizi wa mazungumzo hayo.

Iran imekwishaweka msimamo wake kuwa haitokubaliana na matakwa yasiyotekelezeka  katika mazungumzo na Marekani. Baada ya kuwasilisha mapendekezo ya Iran, Araqchi ameondoka Pakistan na ujumbe wake kuelekea Oman muda mfupi uliopita na baada ya hapo anatazamiwa kuwenda Urusi.