1
1
Shambulizi hilo la anga kutoka Iran linadaiwa kupiga ua wa ubalozi wa zamani wa Marekani. Walioshuhudia wanasema majengo mengine yaliokuwa nje ya ua huo yaliharibiwa vibaya huku vioo vya majengo yaliyokuwa karibu yakipasuka.
Huku hayo yakiarifiwa Israel imetoa onyo kwamba huenda mashambulizi zaidi yakavurumishwa dhidi yake kutoka Yemen na Iran, wakati ikiendeleza mashambulizi yake pia nchini Lebanon yaliyosababisha mauaji ya watu watano.
Hadi sasa hakuna dalili zozote za kumalizika vita hivyo vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Tayari watu 3000 wameuwawa na Rais Trump ameashiria kuwa huenda vita hivyo vikamalizika ndani ya wiki mbili hadi tatu lakini wakati huo huo amekuwa akiamuru maelfu kwa maelfu ya wanajeshi wa Marekani kupelekwa Mashariki ya Kati.
CHANZO: DW