Popular Posts

Iravani akanusha vikali azimio la Arab League dhidi ya Iran, asema ni la upendeleo

Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amejibu azimio la kikao cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab Legue) dhidi ya Iran kilichofanyika mjini Cairo akisema kuwakingia kifua wavamizi hakuwezi kubadili ukweli wa kisheria.

Amir Saeed Iravani amesema haya katika barua aliyomwandikia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Rais wa Baraza la Usalama la Umoja Mataifa, siku ya Jumatatu akisisitiza kuwa majaribio yoyote ya kupotosha ukweli au kuwakingia kifua wavamizi ili wasiwajibishwe hayatabadili ukweli wa kishera wake kuwafanya wahusika wasiwe na majukumu na kuwajibishwa kwa athari mbaya ya kimataifa za uvamizi huo.

Iravani amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga kata kata azimio hilo pamoja na tuhuma za uwongo, za kupotosha na za kisiasa zilizomo. Amesema kuwa azimio hilo linapuuza ukweli usiopingika kwamba Marekani na utawala ghasibu wa Israel, kwa kukiuka vibaya sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa, zimefanya vitendo vya uamizi na mashambulizi ya silaha yasiyo halali na uchochezi dhidi ya mamlaka ya kujitawala na ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

“Badala yake, azimio hilo linajaribu kupotosha historia na ukweli wa mambo, pamoja na mfumo wa kisheria unaotumika, kwa kuishutumu Iran, wakati Iran ndio mwathirika wa vita hivi vya kivamizi visivyo halali,” amesema Iravani.

Balozi Iravani amessitiza kuwa jitihada zozote za kupotosha ukweli au kuwalinda wahalifu wa uvamizi ili wasiwajibishwe hazitabadilisha ukweli wa kisheria wala kuwafanya wahusika wasibebe dhima na kuwajibishwa kwa athari mbaya za kimataifa za uvamizi wao.

 

CHANZO: PARS TODAY