Popular Posts

Marekani kuutathmini upya uhusiano wake na NATO

Rubio alikiambia kituo cha televisheni cha Fox News kwamba Washington inalazimika kuangalia upya thamani ya NATO kwa nchi yake, akiongeza kwamba “uamuzi huo utafanywa na Rais Donald Trump.”

Kauli hiyo ya Rubio inakuja muda mchache baada ya Trump kutumia mtandao wake wa kijamii kuzikosowa vikali Uingereza na Ufaransa ambazo zimekataa kujiunga na vita dhidi ya Iran, zikisema hazikushauriwa kabla.

Badala yake, Trump aliyataka mataifa hayo kujitokeza yenyewe kuufunguwa Mlango Bahari wa Hormuz uliofungwa na Iran kwa meli zote zinazohusishwa na Marekani na Israel ama washirika wao.

Ufaransa iliikatalia Marekani kutumia anga lake kwa ndege zenye silaha kuelekea Israel.

Uamuzi kama huo ulishachukuliwa na Uhispania, ambayo imekataa anga na ardhi yake kutumiwa na Marekani kwa ndege zinazoishambulia Iran.

 

 

CHANZO: DW