Popular Posts

Sheria mpya ya bei za mafuta yaanza Ujerumani

Kupitia kanuni hiyo mpya, vituo vya mafuta vinaruhusiwa kupandisha bei mara moja tu kwa siku, wakati wa mchana.

Kanuni hiyo imeanzishwa ili  kudhibiti upandaji wa bei za mafuta na kuhakikisha kuna uwazi zaidi kwenye biashara ya nishati hiyo muhimu.

Hata hivyo, kanuni hiyo iliyochapishwa kwenye Gazeti Rasmi la Serikali siku ya Jumanne (Machi 31), haikatazi ushushaji wa bei wakati wowote ule.

Hatua hiyo ya Ujerumani inafuatia uamuzi kama huo uliochukuliwa na Austria, ambako imekuwa ikitekelezwa muda mrefu ingawa imetiliwa nguvu zaidi kwenye siku za hivi karibuni.

Vyama vya wenye vituo vya mafuta na kampuni za huduma za magari zinasema huenda kanuni hiyo ikaathiri pakubwa biashara zao.

Watakaobainika kuvunja kanuni hiyo atakabiliwa na faini ya hadi euro laki moja.

 

 

 

CHANZO: DW