Popular Posts

Uganda yapitisha sheria ya ”mawakala wa kigeni”

Wakati wa mjadala mkali bungeni, wabunge hao walipitisha mswada huo baada ya kufutwa kwa kifungu kilichowataja Waganda walio nje ya nchi kama “wageni.”

Mswada huo unaojulikana kama “Mswada wa Ulinzi wa Uhuru” unaharamisha hatua zinazochukuliwa kukuza “maslahi ya wageni kuliko yale ya Uganda” na kuwataja wanaopokea ufadhili wa kigeni kama “mawakala wa raia wa kigeni.”

Watakaopatikana na hatia watakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 20 jela.

Spika wa bunge hilo Anita Among, ameutaja mswada huo kuwa wa kihistoria.

Mbunge Kajwengye Twinomugisha Wilson wa chama tawala amesema kupitishwa kwa muswaada huo ni mafanikio makubwa, huku mwenzake wa upinzani  Gilbert Olanya akisema utaunda mfumo wa vikwazo vikali vya kiutawala vyenya uwezo wa kuathiri uchumi.

 

 

CHANZO: DW