Popular Posts

Ulevi watishia mustakbali wa vijana kijiji cha vikunguni

Na: Nuru Asaa Ali

Kijiji cha vikunguni kinakabiliwa na ongezeko la vitendo vya ulevi miongoni mwa vijana, hali inayozua wasi wasi mkubwa kwa jamii kutokana na athari zake za kijamii na kimaadili

Akizungumza katika mahojiano maalumu, mkaazi wa kijiji hicho Ali  Rashid Khamis amesema kuwa ulevi umekuwa jambo la kawaida kwa vijana wengi kijijini hapo, huku idadi ya wanaojiingiza katika vitendo hivyo ikiongezeka kila siku

Tatizo hili limeenea sana kiasi kwamba limeonekana kuwa ni sehemu ya maisha ya vijana, sababu kubwa ni ukosefu wa juhudi za pamoja katika malezi bora kutoka kwa wazazi na jamii kwa ujumla

Aliongeza kwa kusema kuwa ulevi umekuwa chanzo cha matukio mbali mbali yasiofaa , yakiwemo wizi, vurugu na ukosefu wa nidhamu, kuna vijana  wanaiba mali za watu au kuletwa nyumbani wakiwa wamelewa kupitia kiasi , wengine huwatukana hata wazazi wao bila kujali jambo ambalo hapo awali halikuwahi kushuhudiwa kwa kiwango hiki

Kwa mujibu wa mwanakijiji huyo, hali hiyo pia inaathiri watoto wadogo ambao huiga mienendo hiyo mibaya , hivyo kuongeza hatari ya kuendeleza tatizo hilo kizazi hadi kizazi

Aidha alibainisha  kuwa ongezeko la ulevi linachangiwa na ushawishi wa rika pamoja na wazazi kushindwa kufuatilia mienendo ya watoto wao ipasavyo

Kuhusu suluhisho Ali  Rashid amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wazazi na jamii kwa ujumla katika kusimamia malezi ya watoto

Alipendekaza pia wazazi kutoa taarifa kwa vyombo husika, ikiwemo askari jamii pale wanapobaini watoto wao wameanza kujihisisha na ulevi

Jamii ya vikunguni sasa inahimizwa kuchukuwa  hatua za haraka na za pamoja ili kulinda maadili ya vijana kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho