Popular Posts

UN yawawekea vikwazo makamanda wa RSF Sudan

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limewawekea vikwazo makamanda wanne wa kikosi cha wanamgambo cha Sudan, Rapid Support Forces (RSF), kwa tuhuma za kuhusika na ukatili dhidi ya raia katika mji wa , Darfur Kaskazini. Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema vitendo hivyo vinaonyesha “dalili za mauaji ya kimbari.”

Vikwazo hivyo vinahusisha marufuku ya kusafiri na kufungiwa mali. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema maelfu ya raia waliuawa wakati RSF ilipouteka mji wa el-Fasher Oktoba 26, baada ya kuuzingira kwa miezi 18. Ni asilimia 40 tu ya wakazi 260,000 walioweza kukimbia, huku hatima ya wengine wengi ikiwa haijulikani.

Miongoni mwa waliowekewa vikwazo ni Naibu makamanda wa RSF, Abdul Rahim Hamdan Dagalo na Luteni Jenerali Gedo Hamdan Ahmed, pamoja na Brigedia Jenerali Al-Fateh Abdullah Idris, anayejulikana kama “Abu Lulu.” Ripoti ya kamati ya Umoja wa Mataifa inadai baadhi yao walitoa amri ya kuua raia bila kuwachukua mateka.

RSF, iliyoundwa mwaka 2013 kutoka kundi la Janjaweed, imekuwa vitani na jeshi la Sudan tangu mwaka 2023. Wachambuzi wanasema hatua hiyo ya Umoja wa Mataifa ni muhimu katika kuimarisha uwajibikaji na kuongeza shinikizo la kumaliza mapigano yanayoendelea nchini humo.

 

CHANZO: DW