1
1
Watumiaji wa mitandao ya kijamii wameeleza maoni yao kuhusu vita vya sasa vya Marekani na Israel dhidi ya Iran wakisisitiza kuwa Wairani sasa wamekuwa nembo ya kusimama kidete na kupambana na madola ya kidhalimu na kibeberu kote duniani.
Majibu makali ya Iran dhidi ya uchokozi na mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na mwanasesere wake, Israel, yamewaibua watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii hususan mtandao wa X na kutoa maoni yao kuhusu wanayoyashuhudia sasa katika vita vya kidhalimu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X aliyejitambulisha kwa jina la Kashmala kutoka Pakistan ameandika: Vita vya sasa vimetuonesha kwamba watu wa Iran ndio taifa la tabaka la kipekee la karne ya 21”.
Alon Mirzahi, mwandishi na mchambuzi mashuhuri wa Israel amesema Iran inaendelea kuvurusha maelfu ya makombora na kutuma ndege za kivita zisizo na rubani kila siku dhidi ya Israel na Marekani na kupiga shabaha umbali wa mamia na hata maelfu ya kilomita licha ya kukabiliwa na mashambulizi mazito, lakini hadi sasa haijashambulia hata shule moja. Mirzahi ameandika katika ujumbe mwingine kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba: “Dunia inazama katika kuipenda Iran kama ilivyofanya hapo awali kuhusu Palestina.”
Hamid-Reza Kazemi wa Iran yeye anamini kuwa: Miaka 23 iliyopita Marekani ililishinda jeshi la Iraq na kuiteka Baghdad katika kipindi cha siku 23 tu, lakini sasa jeshi hilo lenye majigambo mengi limenasa katika kinamasi cha Iran. Historia inajirudia: Mara ya kwanza ni maafa na msiba na ya pili ni kichekesho na dhihaka.
Daniel Fox, mchoraji wa Ufaransa pia ameandika katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X: “Iran ni tumaini la dunia. Iran isisitishe vipigo hadi Israel iangamizwe na Marekani ifukuzwe kikamilifu Magharibi mwa Asia. Hivi ni vita kwa ajili ya wanadamu wote. Mustakbali wetu sote unafungamana na Iran.”
Mchambuzi wa masuala ya kijeopolitiki wa Hong Kong, Angelo Juliano, ameandika: Mwaka 2020 Bunge la Iraq lilipiga kura ya kuondoka Marekani katika ardhi ya nchi hiyo. Hata hivyo majeshi ya Marekani kamwe hayakuondoka Iraq. Sasa, Iran inaisaidia Iraq kujikomboa. Hakuna nchi nyingine yoyote inayofikiria kuzikomboa nchi za Kiarabu. Ni Iran pekee ndiyo inayofanya kazi hiyo.”
Solomonko wa Sydney nchini Australia amezungumzia jinsi mlingano wa nguvu unavyobadilika duniani na kuandika: “Siku za nguvu kubwa ya Marekani zimeyoyoma na kuisha. Asante sana Iran.”
Katika sehemu moja ya ujumbe wake, mcheza filamu mashuhuri wa Misri, Amrou Wakid ameashiria jinai ya kuuliwa kigaidi Ayatullah Ali Khamenei na kuandika: Sayyid Ali Khamenei alikuwa mwanasiasa adhimu na shahidi wa njia ya haki ambaye ameiangamiza batili. Amesema: Kuuliwa kwake kumekuwa sababu ya Waislamu kuvurumisha makombora dhidi ya adui ambayo yanaendelea kupiga kambi zote za majeshi ya Marekani katika nchi za Kiarabu. Sisi tunaketi na kutazama kipindi hiki kwa fahari.”
Na mwanablogu wa Kuala Lumpur huko Malaysia, Brofos ameandika: Nafurahi kutoa pesa zaidi kwa ajili ya kununua mafuta ya petroli, gesi, chakula na bidhaa nyingine kwa sababu Iran inashinda vita. Hii ni gharama inayopaswa kutolewa na dunia kwa ajili ya kukomesha dhulma na ubeberu.”
CHANZO: PARS TODAY