Popular Posts

Waziri Mkuu Senegal aapa kuongeza adhabu dhidi ya LGBTQ

Waziri mkuu wa Senegal Ousmane Sonko amezindua sheria ambayo itaongeza maradufu adhabu ya juu zaidi kwa makosa ya mahusiano ya jinsia moja. Watakaopatikana na hatia wataadhibiwa kwa kifungo cha hadi miaka 10 jela.

Watakaopatikana na hatia wataadhibiwa kwa kifungo cha hadi miaka 10 jela ikilinganishwa na kifungo cha mwaka mmoja hadi mitano chini ya sheria ya sasa. Mashirika ya haki za binaadamu yamelaani ukandamizaji huo.

Mawaziri waliuwasilisha muswada huo bungeni baada ya kuupitisha wiki iliyopita, kufuatia kukamatwa kwa watu kadhaa wanaoshutumiwa kuwa na mahusiano ya jinsia moja, kitendo ambacho tayari ni uhalifu chini ya sheria za Senegal. Ousmane Sonko ameliambia bunge jana kuwa “Ikiwa kitendo hicho kitafanywa dhidi ya mtoto mdogo, kitasababisha adhabu ya juu zaidi, ya miaka 10 jela.

Chini ya sheria mpya “kitendo chochote cha ngono au kitendo cha ngono kati ya watu wawili wa jinsia moja kinachukuliwa kuwa kitendo kinachokwenda kinyume na maumbile”.

Polisi mwezi huu walisema waliwakamata wanaume 12, wakiwemo watu wawili mashuhuri nchini humo na mwandishi wa habari maarufu, chini ya sheria zinazopinga vitendo vya mapenzi ya jinsia moja – LGBTQ. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa watu 30 wamekamatwa tangu wakati huo.

 

CHANZO: DW