Popular Posts

Waziri Mkuu wa India alihutubia Bunge la Israel

Narendra Modi ambaye yuko ziarani huko Israel kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya kibiashara na ulinzi, ameongeza pia kuwa India inasimama imara na Israel kufuatia shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023.

” Pia ninawasilisha salamu za rambirambi za dhati kutoka kwa watu wa India kwa kila maisha yaliyopotea na kwa kila familia ambayo iliathirika kufuatia shambulio la kigaidi la Hamas mnamo Oktoba 7, ” alisema Modi.

Waziri Mkuu huyo wa India alikutana na mwenzake wa Israel Benjamin Netanyahu, ziara ambayo imeibua ukosoaji mkali nchini India ambayo kihistoria imekuwa ikiwaunga mkono Wapalestina, lakini sasa kunashuhudiwa mabadiliko ya sera ya kigeni ya India chini ya uongozi wa Narendra Modi.

 

 

CHANZO: DW