1
1
WHO imetangaza uamuzi huo katika Maadhimisho ya Siku ya malaria Duniani Aprili 25, 2026. Shirika hilo limesema dawa hiyo inaweza kusaidia kuziba pengo kubwa la huduma za matibabu kwa takribani watoto milioni thelathini wanaozaliwa kila mwaka katika maeneo yanayoathiriwa na malaria, hususani barani Afrika.
Kabla ya hatua hiyo ya WHO, watoto wengi wachanga walikuwa wakipewa dozi zilizokusudiwa watoto wakubwa. Hali hiyo ili iliongeza hatari ya madhara kwa afya zao.